Mahakama Yaridhia Herbinder Seth Kuletwa Kisutu Jumatatu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Mkurugenzi wa Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia ombi la upande wa Jamhuri la kumpeleka Mkurugenzi wa Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth mahakamani hapo Juni 14, 2021(Jumatatu) ili kuieleza mahakama hiyo mazungumzo yao na mshtakiwa yalipofikiwa.

 

Ombi hilo limeridhiwa na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi leo Juni 11,2021 baada ya wakili wa Serikali Mkuu, Martenus Marandu kuieleza mahakama kuwa wameshafanya mazungumzo na mshtakiwa Seth na Jumatatu wataleta mrejesho.

“Mheshimiwa, mshtakiwa aliandika barua kuhusu hatma ya shauri lake Juni 10, 2021, hivyo tumekubaliana kujielekeza kwenye barua hiyo na tunaomba muda ili tuweze kuifanyia kazi na kama itakupendeza kutoa amri ya kesi hii kuja Jumatatu ili tuitaarifu mahakama makubaliano yetu yamefikia wapi.

 

Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 14, mwaka huu. Mshtakiwa amerudishwa mahabusu.

 

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo, James Rugemalira ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP na Wakili wa kujitegemea, Joseph Makandege wao hawajaonesha nia ya kuandika barua kwa mkurugenzi wa mashtaka nchini DPP hivyo kesi yao itaendelea kama kawaida na itatajwa Juni 17, mwaka huu.

 

Setth na wenzake wanadaiwa kati ya Oktoba 18 ,2011 na Machi 19, 2014 jiji Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad