Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Matumizi ya bangi Rwanda yanapaswa kuidhinishwa na mtaalam

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREAgizo la wizara ya haki nchini Rwanda limetoa muongozo kuhusu matumizi ya bangi nchini humo .
Katika agizo la Jumatatu bangi sasa inaweza kutumika tu inapoagizwa na mtaalamu.

Linasema wawekezaji wanaweza kuomba kupewa leseni ya kufanya kilimo, kuagiza na usafirishaji wa bangi nje ya nchi kwa madhumuni ya matibabu au utafiti.

Amri ya Waziri wa Sheria ilianza kutumika Jumatatu, akielezea jinsi ya kusimamia vifaa vya uchakataji wa bangi nchini Rwanda.

Mwaka jana, serikali ya Rwanda ilipitisha sheria ya kuruhusu kilimo na usafirishaji wa bangi "kwa sababu za matibabu na kifedha".

Bangi ipo kwenye orodha ya dawa haramu nchini Rwanda bado ni haramu na watakaopatikana nayo au kuitumia kinyume na muongozo watadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments