.

6/01/2021

Mbunge alievaa suruali ya kubana aondolewa Bungeni
Mbunge wa Momba Condester Michael Sichalwe ametolewa ndani ya ukumbi wa bunge ili akabadilishe mavazi yake baada ya mbunge wa Nyangw’ale, Hussein Nassor Amar kuomba muongozo wa Spika kuwa kuna baadhi ya wabunge wamevaa mavazi yasio na maadili.
Spika alimtaka mbunge Hussein Nassor Amar kumtaja mmoja ambaye amemuona ndipo alipomtaja Mbunge wa Momba Condester Michael Sichalwe ambapo Spika Ndugai alimtaka atoke ndani ya ukumbi wa bunge ili akabadilishe mavazi yake.

“Spika nasimama kwa kanuni ya  70 inayohusu mavazi ya staha kwa wabunge, kanuni imeeleza  wazi kuhusu mavazi hayo na kwa akina dada lakini humu ndani kuna wabunge wamevaa nguo ambazo hazina staha,” Amar.

Spika Ndugai alimpa nafasi Mbunge huyo kumtaja mwenzake  aliyevaa mavazi ambayo hayakuwa na staha ili iwe mfano.

“Mbunge huyo yuko hapo katika mkono wangu wa kulia, amevalia tisheti  lakini naomba umuite mbele uone suruali aliyovaa namna ilivyobana, amevaa miwani,”  Amar 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger