.

6/08/2021

Rais Samia "Utaratibu wa kuzuia maiti kutoka hospitalini kwa kigezo cha kulipa gharama za matibabu kabla ya kifo si mzuri"
Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuweka utaratibu mzuri ambao hautaleta usumbufu wa uchukuaji wa maiti hospitalini.
Amesema utaratibu wa sasa ambao umekuwa ukizuia kutoa maiti hospitalini kwa kigezo cha kulipa gharama za matibabu kabla ya kifo si mzuri.

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo jijini Dodoma wakati wa mkutamo wake na Wanawake wa Tanzania kupitia Wanawake wa mkoa wa Dodoma.

Amesema ni vema wakati wa matibabu ndugu wa mgonjwa ama mgonjwa mwenyewe akawa anapatiwa gharama za matibabu za kila siku, badala ya kusubiri hadi kifo kinapotokea, na hivyo kuleta usumbufu.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger