.

6/02/2021

Suala la Mbunge Kutolewa Bungeni KISA Mavazi Lazua Utata Bungeni, Mbunge Adai Mbunge Condester Alidhalilishwa


 Mbunge Hussein Nassor: Siombi Radhi

MBUNGE wa Viti Maalum, Jacqueline Ngonyani Msongozi amesimama na kuomba mwongozo kuhusu ishu iliyotokea jana Juni 1, 2021 ya Mbunge wa Momba Condester Michael Sichalwe kutolewa nje ya ukumbi wa Bunge na Spika kwa madai kuwa amevaa nguo zisio na maadili.

Mbunge Msongozi alimtaka Mbunge wa Nyang’wale, Hussein Nassor kuomba radhi akidai kuwa alimdanganya Spika kwa kuwa Mbunge Condester alikuwa na mavazi mazuri.

“Sina nia ya kutoheshimu maamuzi ya Spika kwa lilitokea leo (jana), Mbunge yule alimdanganya Spika, ilikuwa sio rahisi Spika kumwambia Mbunge toka mbele kuangalia vazi lake lakini ukweli ni kwamba Mbunge huyu nguo ni nadhifu na ya heshima na Mbunge huyu mavazi yake ni mazuri.

“Kwa hiyo huyu binti aliyedhalilishwa leo (jana) kwanza ni kijana mdogo na ni mwakilishi wa Jimbo, imeleta taharuki, naomba muongozo wake, huyu Mheshimiwa aliyemdhalilisha mwenzake aombe radhi,” amesema Msongozi.

Mbunge wa Nyang’wale, Hussein Nassor alipewa nafasi na Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson lakini alisimama na kusema hawezi kuomba radhi ambapo wakati akiendelea kufafanua Naibu Spika alimtaka akae chini.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger