.

6/02/2021

Sugu na Msigwa Waliamsha DUDE, Kufungua Kesi Kupinga Unyanyasi MagerezaniPeter Msigwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) ambao wamewahi kukaa gerezani wamesema wanafungua Kesi kupinga unyanyasaji unaoendelea katika magereza ya #Tanzania

Wamesema Tanzania imesaini na kuridhia Mikataba kadhaa kuhusu Haki za msingi za Wananchi ikiwemo Tamko la #HakiZaBinadamu linaloeleza kufungwa hakumfanyi mtu apoteze Haki zake

Unyanyasaji uliotajwa kuendelea kwenye magereza ni pamoja na wafungwa kuvuliwa nguo hadharani, kupewa nguo moja katika maisha yao gerezani, kupangiwa muda wa kwenda haja na kutolipwa kwa kazi zao

Wamesema kutumikia kifungo hakuondoi Utu, bali mfungwa anatakiwa kukosa Uhuru wa kwenda anapotaka. #Haki nyingine zilizoainishwa na #Sheria na Mikataba ya Kimataifa zinaendelea kuwepo

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger