.

6/03/2021

Tanzia: Ismail Michuzi Afariki Dunia

MWANAMUZIKI mkongwe Ismail Issa Michuzi amefariki dunia leo asubuhi Juni 3,  katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar alikokuwa akitibiwa maradhi ya tumbo.

Ismail, ambaye ni kaka yake mpiga picha maarufu na blogger Muhidin Issa Michuzi, amefariki akiwa na umri wa miaka 61.

Ismail atakumbukwa kuwa mmoja wa viongozi na waanzilishi wa bendi ya Dar International chini ya Marijani Rajabu na pia alihudumu kama katibu wa bendi toka mwanzo wake hadi mwisho.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger