.

6/07/2021

Tetesi za Usajili Barani ULAYA Leo Tarehe 07 June


Manchester United wameambiwa kuwa itawagharimu kiasi cha pauni milioni 81.5 kumsajili winga Jadon Sancho,21, kutoka Borussia Dortmund. (Mirror)

Atletico Madrid wanatarajiwa kutoa ofa mpya kwa kiungo wa kati Rodrigo de Paul,27, ambaye pia amekuwa akihusishwa na timu za Liverpool na AC Milan. (Mundo Deportivo- in Italian)

Wolves wnajiandaa kupokea ofa ya Arsenal wiki hii kuhusiana na kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves, 24. (Mail)

Barcelona wamefufua tena mpango wa kumsaka mlinzi wa Manchester City Mhispani Aymeric Laporte, 27, na huenda wakamtoa Sergi Roberto, 29, kama sehemu ya kufanikisha mkataba. (Sport - in Spanish)

Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 34, bado huenda akajiunga na AC Milan, licha ya Chelsea kutangaza mpango wa kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja wiki iliopita. (Goal)

Lazio huenda wakamsajili meneja wa zamani wa Juventus na Chelsea Maurizio Sarri, 62, kama mkufunzi wao mpya wiki hii. (Corriere dello Sport - in Italian)

Afisa Mkuu mtendaji wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi anasema mabingwa hao wa Ufaransa hawatamuuza mshambuliaji wao Kylian Mbappe, 22. (AS - in Spanish)

Aston Villa wako tayari kumnunua kiungo wa kati wa Southampton na England James Ward-Prowse, 26, siku moja baada ya kukubali kuvunja rekodi ya usajili wa klabu hiyo kumsaini kiungo wa kati mwenzake Emiliano Buendia kutoka Norwich. (Guardian)

Itagharimu euro milioni 200 sawa na (paundi milioni 171.8) kumnunua mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20, kutoka Borussia Dortmund msimu huu. (AS - in Spanish)


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger