Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Unaambiwa Wengine Wanuna, Wengine Wakenua Uchaguzi Mkuu TFF

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Wakati Joto la Uchaguzi wa TFF likiendelea kupamba moto, Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka Nchini TFF imepitisha majina matatu kwenye nafasi ya Urais katika mchujo wa awali kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika Agosti 7 mwaka huu Jijini Tanga.

 

Katika taarifa ambayo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Wakili Benjamin Kalume majina yaliyopitishwa katika nafasi ya Urais ni Hawa Mniga,Evans Mageuka na Wallace Karia huku Ally Mayai,Oscar Oscar na  Ally Saleh wameenguliwa kutokana na kutokidhi vigezo vya kanuni za uchaguzi.

''kwa kuwa wanasimamia haki na katiba ya TFF hivyo kwa sasa ni jukumu lao kubandika majina ya wagombea wote ili kujua waliopita kwenye mchujo wa awali huku akiongezea kuwa ni ruksa kwa wagombea kuleta pingamizi lakini mapingamizi yao yawe na mashiko'

Benjamin Kalume makamu mwenyekiti wa uchaguzi  amesema 

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Agosti 7, mwaka huu jijini Tanga ambapo mbali na nafasi moja ya urais, kuna nafasi sita za wajumbe wa kamati ya utendaji zitagombewa.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments