.

6/11/2021

Usajili wa Manyama Azam kama Wijnaldum na PSG

 


Klabu ya soka ya Azam imemtambulisha rasmi mlinzi Edward Manyama kuwa mchezaji wao mpya kwa mkataba wa miaka 3 akitokea Ruvu Shooting.


Manyama ambaye ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ alikuwa anahusishwa kujiunga mabingwa wa soka nchini Tanzania Simba, ili akasaidiane na Mohamed Hussein Tshabalala


Lakini katika hali ya mshangao beki huyo ametambulishwa upande wa Azam ili akasaidiane na Mzimbabwe Bruce Kangwa ambaye kwa sasa uwezo wake unaonekana kupungua siku hadi siku.


Si mara ya kwanza kwa Manyama kuwashangaza watu katika usajili wake, wakati wa dirisha dogo aliondoka ghafla ndani ya kikosi cha Namungo pamoja na kutoa mchango mkubwa kwa timu hiyo kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho akaenda kujiunga Ruvu Shooting.


Suala la Manyama linafanana kwa kiwango fulani na usajili wa kiungo wa zamani wa Liverpool Georginio Wijnaldum kukaribia kujiunga na Barcelona,lakini ghafla akatangazwa upande wa PSG.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger