.

6/03/2021

Wakenya Walishitaki Jeshi la Uingereza Juu ya Moto Uliowaka Nyikani



Mahakama nchini Kenya imewaruhusu wakaazi 1000 wanaoishi karibu na kambi ya mazoezi ya wanajeshi wa Uingereza nchini humo kuomba kulipwa fidia pamoja na shirika moja la mazingira , kuhusu moto wa msituni ulioharibu hekari 4,800 za ardhi.


Moto huo ulianza mwezi Machi katika mbuga ya uhifadhi wanyamapori ya Lolldaiga katika mkoa wa kati wakati wa mazoezi yaliokuwa yakifanywa na wanajeshi hao wa Uingereza.Wakati huo, balozi wa Uingereza nchini Kenya alisema: Uchunguzi kuhusu moto huo uliozuka wakati wa mazoezi hayo yaliokuwa yakiongozwa na wanajeshi wa Uingereza unaendelea .


Lengo letu ni kusaidia kwa dharura jamii iliopo karibu ,tunatumia raslimali zote katika kuudhibiti moto na tunafanya kazi kwa karibu na serikali ya Kenya ili kudhibiti hali.


Kundi moja la mazingira liliwashtaki wanajeshi hao wa Uingereza na usimamizi wa Lolldaiga kuhusu moto huo, likitaka wakaazi wa eneo hilo kulipwa fidia.


Pia lilitaka jeshi la Uingereza na mbuga hiyo ya uhifadhi wa Wanyama kuchukua jukumu la kurudisha mazingira ya eneo hilo.


Kundi hilo lilidai kwamba hakuna mikakati iliowekwa kuzuia moto wakati Wanajeshi hao wa Uingereza walipokuwa wakifanya mazoezi katika eneo hilo.


Wakaazi wa eneo hilo kwa sasa wanaruhusiwa kushiriki katika kesi hiyo.


Mahakama hiyo ya mazingira pia iliambia wakaazi kuchapisha tangazo katika gazeti moja linalowaomba wengine walio na hamu ya kujiunga na kesi hiyo .


Mwezi uliopita , Jeshi la Uingereza liliwasilisha kesi mahakamani likisema kwamba mahakama za Kenya hazina uwezo juu ya suala hilo.


Mahakama haijatoa uamuzi kuhusu ombi hilo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger