Waziri wa Uganda aliyeshambuliwa na watu waliojihami aondoka hospitalini

Waziri wa Uchukuzi na Ujenzi nchini Uganda Jenerali Katumba Wamala ameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa risasi iliyokuwa imekwama kwenye mkono wake.
Bw Wamala alijeruhiwa baada ya watu waliokuwa kwenye pikipiki kulipiga risasi gari lake na kumuua binti yake na dereva.

Waziri Wamala ameomba wote waliohusika na mauaji wakamatwe na kushtakiwa.

Mshukiwa mmoja amekamatwa kuhusiana na mauaji, kulingana na gazeti la New Vision linalomilikiwa na serikali.

Mkesha wa maombolezo ya binti yake waziri Wamala, Brenda Wamala ulifanyika Jumatano usiku. Televisheni ya NTV Uganda ilichapisha video ya waziri akiutazama mwili wa binti yake:

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE