.

6/01/2021

Waziri wa Uganda apigwa risasi na watu wasiojulikana karibu na nyumba yake

Jenerali Katumba Wamala ni Kamanda wa zamani wa jeshiImage caption: Jenerali Katumba Wamala ni Kamanda wa zamani wa jeshi
Jenerali Katumba Wamala, Mkuu wa zamani wa Jeshi la Uganda na Waziri wa sasa wa Ujenzi na Uchukuzi amepigwa risasi na kujeruhiwa na watu wasiojulikana karibu na nyumba yake katika mji mkuu Kampala.

Walioshuhudia wanasema watu hao wenye silaha walikuwa kwenye pikipiki.

Kwa miaka michache iliyopita, nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na mashambulizi kama hayo ya watu wenye silaha wanaoendesha pikipiki.

Mnamo Juni 2018, Ibrahim Abiriga, mwanasiasa shupavu na aliyekuwa mfuasi wa Rais Museveni alipigwa risasi na kuuawa karibu na nyumba yake. Andrew Felix Kaweesi wakati huo akiwa Mkuu wa Operesheni wa Polisi aliuawa kwa njia kama hiyo mnamo Aprili 2017. Hakimu na maulama kadhaa wa Kiislamu waliuawa vivyo hivyo.

Hakuna mauaji yoyote ambayo yamewahi kuchunguzwa kwa mafanikio au washukiwa kushtakiwa


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger