.

6/01/2021

Wema ampigia debe Mondi

Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ambaye pia ni Malkia wa urembo nchini mwaka 2006, amempongeza Msanii wa Bongofleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa kuteuliwa kuwania kuwania tuzo za BET awards.

 

Wema ambaye alikuwa mpenzi wake Mondi, kupitia mtandao wake wa Instagram amemtia moyo Mondi kuwa aende kuchukua tuzo hiyo.

 

Mbali na kuposti picha ya Mondi katika akaunti yake, Wema aliandika “Go Get Em SIMBA…‼️ cc @diamondplatnumz”.

 

Katika tuzo hizo Diamond anachuana na Wizkid, Burna Boy, Emicida, Headie, Aya Nakamura, Youssoupha na Young T & Bugsey.

 

Hii ni mara ya tatu Diamond Platnumz kuchanguliwa kuwania tuzo za BET ambazo zinafanyika Juni 28, 2021. Mwaka 2014 alitajwa kwa mara ya kwanza kuwania tuzo hizo na mara ya pili ilikuwa mwaka 2016.

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger