.

6/08/2021

Yanga Yaweka Mtego kwa Meddie Kagere
YANGA imeiwekea mtego kwa Simba ambao kama ukifyatuka basi itanufaika kwa kuipata saini ya mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere.Mnyarwanda huyo hivi sasa ni mchezaji huru anayeruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine sambamba na kusaini mkataba kutokana na mkataba wake wa kuitumikia Simba kumalizika.

 

Kagere hivi sasa hana furaha na timu hiyo inayofundishwa na Mfaransa, Didier Gomes, kutokana na kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, mabosi wa Yanga wanasubiria kuona hatma ya Simba na mshambuliaji huyo kabla ya kumpa mkataba asaini kukipiga Jangwani.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa mabosi wa Yanga wana matumaini makubwa ya kuipata saini ya mshambuliaji huyo kwa kuwa wameshafuatilia na kugundua kuwa Simba hawajazun–gumza naye jambo lolote hadi sasa huku mkataba wake ukimal–izika mwezi ujao.

 

“Mabosi wa Yanga hivi sasa wamekaa kimya wakisubiria kuona hatima ya Kagere na viongozi wa Simba, kama wakimuacha basi fasta watampa mkataba wa miaka miwili na wanaamini kuwa atakuwa msaada mkubwa.

“Yanga wanaamini bado Kagere ana uwezo mkubwa wa kucheza soka, pia uzoefu wa kucheza Ligi Kuu Bara aliyocheza kwa misimu miwili mfululizo pamoja na michuano ya kimataifa,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Meneja wa Kagere, Patrick Gakumba, hivi karibuni alimvaa kocha wa Simba na kumwambia kuwa: “Sababu kubwa ya kocha wa Simba Gomes kutompa nafasi ya kucheza katika timu ni chuki iliyokuwepo kati yangu na yeye.“Mimi na yeye tulitofautiana baada ya kupata taarifa kuwa nilihusika katika kumnyima kazi kufundisha timu ya taifa ya Burundi, kitu ambacho siyo sahihi.

“Kwanza hakuna kiongozi wa Yanga aliyenitafuta kuongea na mimi juu ya kutaka kufanya kazi na Kagere lakini naamini ni jambo ambalo linawezekana kwani Yanga inapambana kufanya maboresho na mabadiliko makubwa kutokana na historia yake.“

 

Kuhusu mkataba wake na Simba utafikia ukingoni baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu na Kombe la FA baada ya hapo atakuwa mchezaji huru hivyo ikiwa kweli anahitajika na Yanga wanaweza kuja tukaongea.“Hadi jana (juzi), nilikuwa naongea kwenye televisheni ya Rwanda nikasema soka la Tanzania kwa sasa linakuwa kutokana na uwekezaji na Yanga ndiyo wanaelekea huko.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

2 comments:

  1. Our Call Girls in Goa service will provide oral and anal sex facilities also by trained and experienced girls.Call Girls in Goa We have also most of the clients who wish to take these girls for business purposes such that Call Girls in Goa business tour client meetings and presentations also where Call Girls in Goa they can enjoy each and every moment with confidence and they will make his dignity Call Girls in Goa against their business partner. Get Hotel Aloft Aerocity Busty Call Girls

    ReplyDelete

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger