.

6/01/2021

Zinedine Zidane: Real Madrid haikuwa na imani nami

Zinedine Zidane anasema alijiuzulu kama kocha wa Real Madrid kwasababu alihisi klabu hiyo "haina tena imani " naye.
Kocha huyo raia wa Ufaransa aliondoka klabu hiyo ya La Liga kwa mara ya pili katika taaluma yake ya ukocha Mei 27 baada kushindwa kunyakua ubingwa msimu wa 2020 -2021.

Awali, Zidane aliwahi kuwa kocha wa Real kuanzia mwaka 2016-2018 kabla ya kurejea tena miezi 10 baadaye Machi 2019.

"Ninaenda, lakini sio kwamba ninapitiliza, wala isichukuliwe kuwa nimechoka kuwa kocha," amesema Zidane, 48.

Katika barua ya wazi kwa mashabiki, iliyochapishwa na chombo cha habari cha Uhispania cha AS, aliongeza: Ninaondoka kwasababu ninahisi klabu haina tena imani na mimi ninayohitaji, wala ushirikiano wa kujenga kitu katika kipindi cha wastani wala muda mrefu.

"Naelewa soka na ninajua matakwa ya klabu kama Real Madrid. Najua usiposhinda, unahitajika kuondoka.

"Mimi ni mshindi wa kuzaliwa na nilikuwa hapa kwa ajili ya kushinda mataji, lakini muhimu zaidi ya hili, ni watu, hisia zao, maisha yenyewe na ninahisi haya hayajazingatiwa.

"Kumekuwa na kutoelewa kwamba mambo haya pia ndio chanzo kikuu cha klabu kikubwa. Kwa kiwango fulani, nimekosolewa kwa hilo."

Aliyekuwa mchezaji wa Ufaransa, ambaye alichezea Real kuanzia mwaka 2001 hadi 2006, alishinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa mara tatu na Ligi ya La Liga katika kipindi chake cha kwanza kama kocha.

Alipata ubingwa wa pili wa Ligi ya La Liga mwaka 2019-20 na alikuwa na mwaka mmoja uliosalia katika kandarasi yake kipindi kilichosalia alipoondoka.

Zidane amesema kuwa miaka 20 akiwa Bernabeu ilikuwa "ndiyo kitu kizuri zaidi kuwahi kumtokea" maishani mwake na kwamba "ataendelea kuwa mwingi wa shukrani "kwa rais wa Real Florentino Perez.

"Nataka kuwe na heshima kwa kile tulichofikia. Na pia ningependa uhusiano wangu na klabu na rais katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita kuwa tofauti kidogo ikilinganishwa na makocha wengine," Zidane ameongeza.

"Sikuwa ninaomba kuwepo na upendeleo, hapana, badala yake kuwepo na kumbukumbu. Siku hizi maisha ya kuwa kocha katika klabu kubwa ni misimu miwili, ama kidogo tu ya hapo.

"Ili idumu zaidi uhusiano wa kibinadamu ni lazima, ni muhimu hata zaidi ya pesa, umaarufu au zaidi ya kingine chochote kile. Yanahitaji kukuzwa.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger