.

7/30/2021

Aliyemuua Askari Arusha afariki akijaribu kuwatoroka PolisiJambazi aliyemuua kwa kumkata mapanga Askari, H.2407 Constable Damasi Magoti wa kituo cha Polisi Mbughuni Wilayani Arumeru, Jacob Kideko au Ramadhani Kichwa(43) Mkazi wa Makiba amefariki dunia katika jaribio la kuwatoroka Polisi alipokuwa akisafirishwa jijini Arusha.


Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, jambazi huyo alikamatwa July 27 ,2021 Mkoani Morogoro alikokuwa amejificha kukwepa Polisi na walipofika eneo la Kisongo jijini Arusha akiwa kwenye gari amefungwa pingu mkononi alijaribu kuruka kuwakimbia Polisi.


Taarifa hiyo inadai kwamba mtuhumiwa alipata majeraha kichwani na michubuko kwenye mwili wake, Hata hivyo Polisi walijaribu kuokoa Maisha yake kwa kumpeleke katika hospital ya Mkoa Mount Meru ,lakini alipoteza maisha akiwa njiani.


Inadaiwa kuwa jambazi huyo alikuwa akisakwa na Askari wa gereza kuu la Arusha baada ya kufungwa miaka 16 ,September 10 ,2008 lakini alitoroka mnamo April 1, 2017 akiwa chini ya ulinzi wa askari wa Magereza.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger