.

7/26/2021

Breaking News: Mbowe Afikishwa MahakamaniMWENYEKITI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na kusomewa mashtaka yanayomkabili leo Jumatatu, Julai 26, 2021. Taarifa kutoka CHADEMA zinasema Mbowe alifikishwa mahakamani kimyakimya bila familia yake kujua wala wakili wake.

Kiongozi huyo wa chama hicho, kikuu cha upinzani nchini, alitiwa mbaroni alfajiri ya kuamkia Julai 21 akiwa hoteli ya Kingdom mtaa wa Ghana alikokifikia kwa ajili ya kushiriki kongamano la Katiba Mpya lililoandaliwa na Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha).

Hata hivyo, siku iliyofuata Msemaji wa Polisi nchini, David Misime aliueleza umma kuwa Mbowe anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi na kuua viongozi wa Serikali.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger