.

7/30/2021

Diamond kukusanya Sh1.78 bilioni kwa Shoo 11 atakazofanya Marekani
Dar es Salaam. Mwanamuziki wa Bongofleva kutoka WCB, Nasib Abdul maarufu Diamond Platnumz anatarajia kuanza ziara ya kimuziki nchini Marekani ambapo atafanya shoo 11 kuanzia Oktoba 8 hadi 31, 2021.


Kwa mujibu wa DMK Global Entertainment, sehemu atakazofanya shoo  ni pamoja na Atalanta, Washington DC, Seattle, Minneapolis, Los Angeles, New York, Louisville, Arizona, Boston, Houston na Dallas.


Tayari msanii mwingine wa Bongofleva, Harmonize naye ametangaza kuanza ziara yake nchini humo kuanzia Agosti 28, 2021 ambapo ataanzia katika jimbo la Ohio.

Hivi karibuni meneja wa Diamond, Sallam SK alisema msanii huyo anatoza dola70,000 sawa na Sh162.2 milioni kwa shoo za nje, huku Zuchu ikiwa ni dola20,000 sawa na Sh46.3 milioni.


Kwa muktadha huo, katika shoo hizo 11, Diamond anaweza kuingiza takribani Sh1.78 bilioni ikiwa kila moja atatoza Sh162.2 milioni kama alivyoeleza Sallam SK.


Ikumbukwe Aprili, 2020 Diamond alisema alikuwa amepata hasara ya Sh3.5 bilioni kutokana na kuaihirishwa kwa shoo zake alizotarajia kuzifanya katika nchi zaidi ya 10 kufuatia mlipuko wa virusi vya corona duniani kote.  


Diamond anarejea Marekani ikiwa ni takribani miezi miwili tangu akanyage nchini hiyo alipohudhuruia hafla ya utoaji tuzo za BET 2021 alipokuwa anawania kipengele cha Best International Act na ushindi kwenda kwa Burna Boy wa Nigeria
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger