.

7/29/2021

Kesi Yake na Yanga, Morrison Aomba Mashabiki WamuombeeHayawi hayawi sasa yamekuwa, Jaji Patrick Stewart kutoka Uingereza hii leo ataisikiliza kesi ya Mabingwa wa Kihistoria Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans Sports Club dhidi ya mchezaji Bernard Morrison kabla ya kuitolea uamuzi.

 

Mwanasheria wa Yanga, Simon Patrick amesema hawezi kuzungumza chochote hadi kesi hiyo itakaposikilizwa. Morrison kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram amewataka wafuasi wake kumuombea na waliomtakia kila lakheri ni pamoja na CEO Barbara Gonzalez.

 

Ujumbe wa Bernard Morrison kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram; ”Even in the abundance of water , the fool will still be thirsty ๐Ÿคฆ๐Ÿฝ‍♂️. Wish me well today ๐Ÿ’ช๐Ÿพ๐Ÿ™ akimaanisha kuwa “hata kwenye maji mengi, mjinga huhisi kiu.”

 

Ikumbukwe kuwa, Kesi ya Yanga dhidi ya Morrison katika mahakama ya CAS inasikilizwa leo, hivyo wadau wa soka wapo macho kusikilizia nini kitaamriwa katika shauri hilo ambalo Yanga wanadai Morrison alisajiliwa SImba Sc wakati akiwa na makata halali na Yanga.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger