.

7/26/2021

Kumekucha.. Mbowe ashtakiwa uhujumu uchumu, njama za ugaidi
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka ya uhujumu uchumi ambayo ni kula njama na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili shughuli za ugaidi.

Mbowe amefikishwa mahakamani hapo leo, Jumatatu Julai 26, 2021 na kusomewa mashtaka yake na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ester Martin akisaidiana na Tulimanywa Majigo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Miongoni mwa mashtaka hayo, Mbowe anadaiwa Kati ya Mei na Agust, 2020 katika hoteli ya Aishi iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro, mshtakiwa alikuwa njama za Kutenda kosa Kinyume na sheria.

Upelelzi wa Kesi hiyo umekamilika na upande wa Mashtaka umeileza Mahakama kuwa unaomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasilisha nyaraka muhimu Mahakama Kuu kwa Kusomewa Maelezo ya mashahidi na vielelezo( Commital Proceedings).


Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 5, 2021 ambapo upande wa mashtaka watawasilisha nyaraka Mahakama
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger