.

7/29/2021

Majanga.. Ateketea kwa Moto Gesti
MTU mmoja mkoani Kagera aliyetajwa kwa jina la Neema Bayo (49) aliyekuwa ndani ya moja ya vyumba vya nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Anti iliyoko wilayani Muleba mkoani Kagera amepoteza maisha kwa kuteketea kwa moto ulioteketeza nyumba hiyo ambao hadi sasa chanzo chake hakijajulikana baada ya kushindwa kujiokoa.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo Kamishina Msaidizi, Revocatus Malimi alifika kwenye eneo la tukio na kupata maelezo ya awali kutoka kwa mhudumu wa hoteli hiyo.

Baada ya kupata maelezo hayo akielezea juu ya tukio hilo amesema kuwa marehemu huyo alikuwa ni mmoja wa watu watano walikuwa wamefikia kwenye nyumba hiyo ya wageni ambao walinusurika kifo baada ya kujiokoa kufuatia moto huo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger