.

7/27/2021

Majibu ya serikali kuhusu tozo za miamala kutolewaMsemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kuwa suala la tozo za miamala ya simu limeanza kufanyiwa kazi na kwamba taratibu zinakamilishwa na hadi kufikia mwisho wa mwezi Julai serikali itatoa majibu juu ya suala hilo.

Ujumbe huo umeandikwa hii leo Julai 27, 2021, kupitia ukurasa wa mtandao wa Twitter wa Msemaji Mkuu wa Serikali, zikiwa zimepita siku kadhaa tu tangu Rais Samia Suluhu Hassan, atoe maelekezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, kuhakikisha wanashughulikia malalamiko ya wananchi kuhusu tozo za miamala.

Tozo ya uzalendo katika miamala ya simu kwa mtumaji ama mpokeaji wa pesa zilianza kutozwa Julai 15 mwaka huu, ambapo kufuatia hatua hiyo wananchi walianza kulalamika kwani makato ni makubwa ikilinganishwa na yale ya awali yaliyokuwa yamezoeleka.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger