Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Manara "Nitatimiza ahadi yangu ya Kumpa Mzee Mpili Milioni Moja Jumatano"

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Haji Manara amekubali kutimiza ahadi ya kumpa Mzee Mpili Shilingi Milioni Moja.

Haji aliahidi kumpa Mzee huyo aliejizolea umaarufu mitandaoni kufuatia uzalendo kwa klabu yake ya Young Afruvans, baada ya kumuahidi kufanya hivyo endapo Young Africans ingeifunga Simba SC.

Manara amesema atatimiza ahadi hiyo atakaporejea jijini Dar es salaam siku ya Jumatano (Julai 07).

“Kwa sasa nipo safari, nitatimiza ahadi yangu ya kumpa Mzee Mpili Shilingi Milioni Moja Cash, nitakaporejea Dar es salaam keshokutwa Jumatano.”

“Niliahidi lazima nitimize, siwezi kufanya hiyana kwa mzee kama Mpili, wameshinda dhidi yetu, hivyo anastahili nilichomuahidi.” Amesema Manara

Simba SC ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Young Africans Jumamosi, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments