.

7/24/2021

Mrembo Mkali Adaiwa Kuua Sponsar WakeMIONGONI mwa visa vizito vilivyojiri wiki iliyopita, kipo kisa cha mmoja wa warembo ambao siku hizi wamepewa jina la ‘pisi kali’ kutokana na uzuri wao aliyetambulika kwa jina la Chidinma Ojukwu Adaore mwenye umri wa miaka 21.

Chidinma ambaye ni mwanafunzi wa Shahada ya Mawasiliano ya Umma (Mass Communication) katika Chuo Kikuu cha Lagos nchini Nigeria, anadaiwa kumuua mwanaume aliyekuwa anamuweka mjini (danga lake) aitwaye Usifo Ataga ambaye ni mkurugenzi wa kituo cha televisheni.

ALIPANGIWA APARTMENT

Katika tukio hilo la wiki iliyopita, ripoti za awali zinadai kwamba, mshukiwa wa kwanza kwenye tukio hilo la mauaji ni Chidinma ambaye wakati anapangiwa ‘apartment’ na mwanaume huyo alitumia jina feki la Jewel.

Tukio hilo limejiri kwenye ‘apartment’ hiyo aliyopangiwa Chidinma katika Mtaa wa Adebowale Oshin, Lekki Phase I huko jijini Lagos nchini Nigeria.


Kwa mujibu wa maelezo ya awali aliyoyatoa Chidinma baada ya kutiwa mbaroni na Jeshi la Polisi nchini humo, wakati tukio hilo la mauaji ya mwanaume huyo anayekaridiwa kuwa na umri zaidi ya miaka 40 yanajiri, yeye alikuwa ametumia madawa ya kulevya hivyo hakumbuki hasa ni nini kilichotokea.

AKIRI KUMCHOMA KISU

Hata hivyo, baada ya kubanwa na maswali, Chidinma amekiri kumchoma kwa kisu mara nyingi mpenzi wake huyo.

Pia Chidinma amekiri kwenda benki na kutoa pesa za mwanaume huyo kwenye ATM baada mauaji hayo ambapo alinaswa kwenye kamera za CCTV.


Chidinma alikiri hayo baada ya kubanwa kwelikweli kwenye Kituo Kikuu cha Polisi cha Ikeja jijini Lagos ambapo pamoja na kukiri kutumia madawa ya kulevya, pia alikiri kuwa wawili hao walikuwa wamelewa lilipojiri tukio hilo.

VITU/ MAJINA FEKI

Baadhi ya majina au vitu feki vilivyoongeza shaka juu ya Chidinma ni pamoja na hati ya kusafiria ya Nigeria (passport) yenye namba B50010434, leseni feki ya gari yenye jina la Mary Johnson, lakini ikiwa na picha ya mrembo huyo na kadi ya Benki ya UBA (United Bank for Africa) yenye jina lake na kitambulisho cha chuo (UNILAG identity card).

Ripoti hiyo ya Polisi imeeleza kuwa, baada ya kutekeleza unyama huo, Chidinma alikwenda kukodi chumba katika hoteli moja kwa kutumia jina feki la Jewel ambalo amekuwa akilitumia kwenye shughuli zake nyingine za upigaji.

Imeelezwa kwamba, siku ya tukio, mwanaume huyo alifika kwa Chidinma ambapo kesho yake ndipo iligundulika kwamba, ameuawa baada ya mfanyakazi kuingia kwenye chumba cha mrembo huyo kwa ajili ya kufanya usafi.


 
DAMU ZATAPAKAA CHUMBANI

Tukio hilo liliripotiwa Polisi na msimamizi wa apartment hiza bibi Nkechi Mogbo.

“Mfanya usafi alipoingia chumbani kwa ajili ya kufanya usafi ndipo akagundua mwili wa Ataga ulikuwa umelala chini; sehemu iliyotapakaa damu.

“Uchunguzi wa kina unaendelea kwa ajili ya kufikishwa mahakamani,” ilisema sehemu ya taarifa ya Polisi juu ya tukio hilo.

FUNZO KWA WANAUME

Kisa cha Chidinma kimeendelea kuibua mijadala kemkem kwenye mitandao ya kijamii ambapo kubwa ni kwamba, wanaume wanapaswa kuchukua tukio hilo kama somo kwani baadhi ya mabinti wanaoishi kwa kutegemea masponsa wanachoangalia ni pesa tu na siyo uhai wa mtu.


STORI; SIFAEL PAUL NA MTANDAO
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger