Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Nay wa Mitego Ajuta "Sitaki Kujionyesha Tena Kuwa Nina Hela na Mali"

 


Nay wa Mitego amesema amejifunza mambo mengi hivyo hataki kuyaonyesha maisha yake kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa mwanzo akifanya 'show off' za mali zake kama gari, nyumba  au hata mpenzi wake.

NEW GOVERNMENT JOBS CLICK HERE

Msanii huyo amesema hivyo kwa sababu anaamini mashabiki wake wengi ni wale wa hali ya chini na wa mtaani hivyo hataki kuwaumiza roho kwani bado anahitaji sapoti yao kwenye shughuli zake za kimuziki.

"Sitaki kujionyesha tena watu wanajua kama nafanya muziki sipendi ku-show off, watu wanaonisapoti kula yao ni shida lakini wananipenda, mashabiki wangu wengi asilimia kubwa ni walala hoi, watafutaji, wamachinga wanamaisha ya kuungaunga sitaki kuwaumiza roho bado nahitaji sapoti yao" ameeleza Nay wa Mitego 

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments