Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Neno la Mwisho la Aliyeuawa kwa Risasi SinzaMdogo wa Marehemu Gift Mushi, Edga Kombe
Mdogo wa Marehemu (Gift Mushi) analiyeuawa kwa kupigwa risasi Sinza mkoani Dar es Salaam, Edga Kombe ameleezea neno la mwisho la kaka yake kabla ya umauti kumfika.

Kombe ambaye ni mdogo wa marehemu upande wa baba mdogo amesema marehemu kabla ya umauti alisema “ntakuzika na wewe unizike”.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Julai 18,2021 Kombe amesema “ntamzika ndugu yangu kwa sababu alisema nimzike ninatimiza ahadi, hii yenyewe ni cheni yake nilimvua mochwari tulivyokuwa tunamsafisha.”

Tukio la mauaji lilitokea jana Julai 17, majira ya saa kumi na moja jioni likimuhusisha kijana Alex Korosso ambaye alimpia risasi sita maeneo tofauti Gift Mushi kisha na yeye kujiua kwa kujipiga kwa risasi.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments