Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

RC Makalla aagiza mabasi yote kupakia na kushusha abiria stend kuu mbezi louis

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amelielekeza Jeshi la Polisi kuhakikisha kuanzia sasa mabasi yote yanashusha na kupakia abiria kwenye kituo kikuu cha mabasi cha Mbezi Louis.

RC Makalla amesema hayo leo alipotembelea kituo hicho na kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za Wafanyabiashara kituoni hapo.Amesema Serikali inatambua kituo kimoja pekee cha Mabasi cha Mbezi na uwekezaji uliofanyika ni mkubwa hivyo hakuna maana kama kila mmiliki wa mabasi atakuwa na kituo chake cha kupakia na kushusha abiria.


Aidha RC Makalla ameelekeza uongozi wa Stendi hiyo kuweka utaratibu wa baadhi ya Mabasi kushusha abiria kwenye eneo la kulaza magari ambapo kuna banda la Mamalishe ili kuchochea biashara.
Kuhusu changamoto ndogondogo zilizojitokeza kituoni hapo, RC Makalla ameelekeza viongozi wa Halmashauri ya Ubungo na kituo kuzipatia ufumbuzi wa haraka.

RC Makalla pia ameelekeza Wafanyabiashara kituoni hapo kupangwa katika utaratibu mzuri na bora kwa kuendana na hadhi ya kituo. 

Wakati huohuo RC Makalla ametembelea Soko la Machinga lililopo pembezoni mwa Stendi hiyo na kutaka wafanyabiashara wote wahamishiwe sokoni hapo na uchunguzi ufanyike kwa wale waliopatiwa vibanda kwa upendeleo na kujuana ambapo Wafanyabiashara hao wamesema wapo tayari kuhamia sokoni hapo kwa kuchoka kufanya biashara barabarani.

Aidha amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kuweka utaratibu wa Daladala kushusha abiria sokoni hapo ili kuchagiza biashara.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments