.

7/26/2021

Rooney aripoti polisi baada ya picha chafu kusambaa mtandaoniMchezaji wa zamani wa England, Wayne Rooney ameripoti polisi baada ya kupigwa picha za faraga na watu wasiojulikana, wamesema mawakili wake.Picha ambazo zilisambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii, zinamuonesha Bw Rooney akiwa amelala kwenye kiti huku akiwa na wanawake kando yake.

Haijulikani ni lini picha hizo zilipigwa na hakuna ushahidi kuwa Rooney alikuwa na mienendo yoyote isiyofaa.

Mawakili wa nyota huyo wa zamani wa Manchester United wamethibisha kuwa suala hilo limeripotiwa kwa polisi.

Mawakili wake wamekataa kuzungumzia kuhusu chanzo na asili ya picha hizo. Wakati Polisi ya Greater Manchester imeombwa kuzungumzia suala hilo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger