.

7/26/2021

Shabiki wa Simba Afariki Dunia Kisa Yacouba wa Yanga


Shabiki wa Simba, Kilosa Said (50+) wa Kijiji Cha mwamgongo (mwambao wa ziwa Tanganyika ) Mkoani, Kigoma amefariki Jana wakati akiangalia mpira wa Simba na yanga.

Rafiki wa Marehemu, Msafiri Ismail Shibu, amesema tukio hilo lilitokea walipokuwa wakiangalia mchezo huo wa Derby kwenye ‘Screen’ eneo la Mwamgongo.

“Tulikuwa tunaangalia mpira eneo la Mwamgongo, tulitandika turubai chini tukawa tunaangalia mpira kwenye `screen’ wakati Mchezaji wa Yanga, Yacouba SongnĂ© anafanya shambulizi kwenye lango la Simba presha ikapanda.

“Tukamchukua na kumpeleka hospitali, akawa ameshapoteza maisha, presha yake ilikuwa 250, Marehemu ameacha mke na watoto wawili,” Msafiri Ismail Shibu.

Kilosa anatarajia kuzikwa leo Julai, 26 saa 10, jioni katika kijini cha mwamgongo, mkoani Kigoma.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger