Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Shinyanga Yakanusha Kuzidiwa na Wagonjwa wa Corona na Upungufu Mitungi ya Oksijeni

 


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati, amekanusha uvumi uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, kuwa mkoa huo ume zidiwa na wagonjwa wa COVID-19 na una upungufu wa mitungi ya Oksijeni na kuitaka jamii kuupuuza uzushi huo.

 

Akizungumza na watumishi wa umma, Mkuu wa mkoa huo amesema kuwa watachukua hatua kali kwa mtu aliyehusika kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii kuwa hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga imeelemewa na wagonjwa  wa COVID-19.


Aidha RC Sengati akatumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya Corona kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments