Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Simba Yanyukwa na Yanga Mbele ya Rais Samia 1-0
TIMU ya Wananchi Yanga imefanikiwa kuiduwaza Simba mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuicharaza kwa bao 1-0, mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mkapa Dar es salaam.

 

Yanga ambao walianza kwa kasi tangu dakika ya kwanza, wakifanikiwa kupata kona na nafsi kadhaa za kufunga ambazo washambuliji wa Yanga wangekuwa makini hali ingekuwa tofauti.

 

Goli la pekee katika mchezo huo wa watani wa jadi limewekwa kimiani na kiungo Zawadi Mauya dakika ya 12 kutokana na mpira wa kona kuzagaa kwenye nje ya 18.

 

Kwa matokeo hayo Yanga imefanikiwa kuizua Simba kutangaza ubingwa na baada ya kichapo hicho, Yanga imefikisha alama 70 baada ya kucheza michezo 32, Simba bado wanaoongoza ligi kwa Alama 73 wakicheza michezo 30.

 

Aidha mechi hiyo imehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.


 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments