.

7/29/2021

Steve Nyerere Kuhusu Manara: Maadui ni Wengi

MSANII wa filamu Steven Mengere maarufu kama Steve Nyerere amedondosha comment yake baada ya taarifa iliyotolewa na Klabu ya Simba kuhusu kuachana na aliyekuwa Msemaji wa Klabu hiyo, Haji Manara kwa kusema hakuna jambo lisilokuwa na mwisho.

 

Kupiti ukurasa wake wa Instgram Steve Nyerere ameandika ujumbe mzito kwenda kwa Manara; “Rafiki inatosha kusema kila jambo lina mwanzo na mwisho, umefanya makubwa kwenye Simba, hakuna mashabiki wa Simba wasiojua ulicho kifanya, ulijitoa kwa moyo wako wote, sio rahisi sana watu wote kujua uliyokuwa unapitia lakini kama akijua Mungu na familia yako inakupasa kusema asante.

 

“Unakwenda kupumzika ukiwa umejenga uwezo mkubwa kwenye mpira, wewe ni binadamu lazima kwa nafasi uliyokuwa nayo maadui ni wengi kuliko watu wema, pokea na sema asante kwa kila jambo, uzuri wako hujawahi kubagua rafiki kwa kuchagua Yanga, Mtibwa, au Lipuli.

 

“Tanguliza kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho na maliza kwa kusema shujaa hana thamani kwao, unabaki kwenye midomo ya watu, utaishi kwenye mifano mingi kwenye kila jambo la Simba, utakumbukwa na mkatokeo, Pumzika mdogo wangu, rafiki yangu kipenzi haina shida tuna kesho nyingi kuliko leo,” amesema Steve Nyerere.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger