Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Taarifa za Kukamatwa Mganga wa Kienyeji Aliyeshawisha Ukatili wa Mtoto Mdogo Arusha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP- Justine Masejo akiongea na waandishi wa habari leo amesema Tarehe 08.07.2021 muda wa 07:00 mchana huko maeneo ya Sombetini katika Jiji la Arusha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha lilimkamata na linaendelea kumhoji mganga wa kienyeji (jina limehifadhiwa) mkazi wa Sombetini jijini Arusha kwa tuhuma za kumshawishi mtuhumiwa wa tukio la ukatili dhidi ya Mtoto lililotokea tarehe 06 Julai mwaka huu eneo la Burka.

Amesema kuwa tarehe 08 Julai mwaka huu tulitoa taarifa ya mtoto wa kiume mwenye miaka (4) ambaye alifanyiwa ukatili wa kipigo pamoja na kuwekewa majani mdomoni na baba yake wa kufikia na kutekelezwa katika eneo la Burka.

Kammda masejo amewaambia waandishi wa habari kuwa Katika mahojiano ya kina na mganga huyo wa kienyeji mkazi wa sombetini ambaye amekiri kumshawishi mtuhumiwa huyo aliyemfanyia ukatili mtoto wa miaka minne (04) ambapo alimshawishi kwamba ukifanya kitendo hicho kitamsaidia katika kesi zake pamoja na utajiri katika biashara.

ACP Masejo ameendelea kusemea Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea na Upelelezi pindi utakapokamilika Jalada litapelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua za kisheria.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments