Taarifa za mtuhumiwa aliyetoa taarifa za kutekwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP JUSTINE MASEJO Akiongea na waandishi wahabari leo ofisi kwake amesema kuwa Mnamo 25.07.2021 muda wa saa 15:20 Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha lilipokea taarifa kutoka kwa mtu mmoja (jina limehifadhiwa) kuwa ndugu yake aitwaye DICKSON S/O PETER MUNGULU ametekwa ambapo taarifa hizo walizipata kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS) uliotumwa kutoka kwa simu ya mhanga ukieleza kwamba ametekwa na ili aachiwe zinahitajika kiasi cha fedha Shilingi Milioni Tatu (Tsh.3,000,000) vinginevyo atauawa.

Amesema kuwa Baada ya kupokea taarifa hizo Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilifanya uchunguzi wa kina na tarehe 28.07.2021 muda wa jioni Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilifanikiwa kumpata Kijana huyo aliyesadikika kuwa ametekwa huko maeneo ya MOROMBO katika nyumba ya kulala wageni (Jina limehifadhiwa).

Kamanda wa Polisi ameendelea kuwaambia waandishi kuwa Baada ya kumhoji DICKSON S/O PETER MUNGULU ambaye mwaka 2020 alimaliza Shahada ya Elimu katika Chuo kikuu cha Makumira kilichopo Arusha, ilibainika kuwa alitoa taarifa za uongo kwa ndugu zake ili pate kiasi hicho cha fedha ziweze kumsaidia kulipa madeni yake mbalimbali yanayomkabili.

ACP MASEJO amesema kuwa Sambamba na hilo baada ya kumchunguza zaidi katika mwili wake ilibainika kuwepo na majeraha sehemu ya Shingo na Mguu alikiri kujichoma na kitu chenye ncha kali yeye mwenyewe kwa nia ya kuuaminisha wazazi wake pamoja na ndugu zake wengine kwamba alitekwa.

Jeshi la Polisi Mkoani hapa linaendelea na upelelezi wa tukio hilo na pindi utakapokamilika jalada litapelekwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali kwa hatua zaidi za kisheria.

Kamanda Masejo ametoa wito kwa wananchi,vijana wenye tabia kama hii ilionyeshwa na kijina uyu kuwa Jeshi la Polisi halita wafumbia macho wale wote watakao husika na litawachukuliwa hatua kali za kisheria kwa wataobainika kupotosha umma na kutoa taarifa za uzushi kwa kwa jamii.Pia niwaombe wananchi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo yao kwa Jeshi la Polisi ili zifanyiwe kazi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad