'Tapeli Tajiri' Hushpuppi Akutwa na Hatia ya Makosa ya Utakatishaji edha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Mtu mashuhuri katika mtandao wa Instagram raia wa Nigeria Hushpuppi, ambaye jina lake halisi ni Ramon Abbas, amekiri kosa katika mahakama nchini Marekani la utakatishaji fedha
Alikamatwa, sambamba na washukiwa wengine, huko Dubai mwezi Juni mwaka jana kwa shutuma za ulaghai wa kiasi cha dola milioni 1.1 za Marekani zinazohusishwa na ufadhili wa shule.

Hushpuppi alirejeshwa Marekani ili kuyakabili mashtaka dhidi yake.

Nyaraka zake za kujibu mashtaka zimeonesha kuwa alikiri kuhusika katika sakata ya ufadhili wa shule na vitendo vingine vya ulaghai ikiwemo kinachojulikana kama barua pepe za kibiashara na kuwahadaa watu kupitia mitego iliyohusisha dola milioni 24 taarifa ya Ofisi ya mwendesha mashtaka marekani imesema.

Hati yake inaonesha kwamba alikiri kuhusika katika mpango wa fedha za shule na kama shughuli zingine za ulaghai, pamoja na ile inayojulikana kama mipango ya biashara ya barua pepe, ambayo ilifikia $ 24m, taarifa kutoka Ofisi ya Wakili wa Merika inasema.

Taarifa imeongeza kuwa Hushpuppi alishirikiana na raia wa Kenya na Nigeria kwenye udanganyifu huo wakijifanya washauri na wafanyakazi wa benki kumtampeli mfanyabiashara wa Qatar.

Hushpuppi alikuwa maarufu sana kwenye mtandao wa Instagram kutokana na mtindo wake wa maisha ya kifahari akimiliki magari mbalimbali ya kifahari.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad