Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Uingereza yatinga nusu fainali ya Euro 2020
Uingereza imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Euro 2020 baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Ukraine usiku wa Jumamosi Uwanja wa Olimpico Jijini Roma nchini Italia na sasa itakutana na Denmark Jumatano.

Mabao ya Three Lions yamefungwa na Harry Kane mawili dakika ya nne na 50 na Harry Maguire dakika ya 46 na Jordan Henderson dakika ya 63.

Mchezo uliotangulia Denmark iliichapa Jamhuri ya Czech 2-1 Uwanja wa Bakı Olimpiya Jijini Baku nchini Azerbaijan. Mabao ya Denmark yamefungwa na Thomas Delaney dakika ya tano na Kasper Dolberg dakika ya 42, wakati la Czech limefungwa na Patrik Schick dakika ya 49.

Nusu Fainali ya kwanza itazikutanisha Italia na Hispania Jumanne, wakati England na Denmark zitaumana Jumatano, mechi zote zikichezwa Uwanja wa Wembley Jijini London kuanzia Saa 4:00. 

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments