Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Watuhumiwa dawa za kulevya kortini
Watuhumiwa wa dawa za kulevya ambao ni wakazi wa Mbagala Kuu, George Mwakang’ata (38) na wenzake wawili wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shitaka la kusafirisha kilogramu 1.2 za dawa za kulevya aina Heroin.


Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Andrew Paul Paul wa Kurasini (34) na Said Mgoha Mkazi wa Mtoni Kijichi Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam.

Akisoma mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Rita Tarimo, wakili wa serikali Yusuf Aboud amesema kuwa washitakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Juni 21 mwaka huu eneo la Mivinjeni, Temeke Dar es Salaam.

Wakati huo huo washitakiwa hao walikutwa wakisafirisha kilogramu 1.2 za dawa za kulevya aina ya Heroin.

Kwa upande wa mashitaka ilidaiwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kesi iliahirishwa hadi Julai 27 mwaka kwa ajili ya kutajwa.

Aidha Watuhumiwa walipelekwa mahabusu kwakuwa shitaka lililoko mbele yao halina dhamana na hawakutakiwa kujibu lolote kwakuwa mahakama hilo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.


 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments