Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Zari Ampiga Kibuti King Bae
KIMEUMANA, ndivyo unavyoweza kutafsiri kile alichofanya Mzazi mwenza wa staa wa Bongofleva nchini, Diamond Platnumz, Zarina Hassan maarufu kama ‘Zari the boss lady’ baada ya kufuta picha zote alizopiga pamoja na mpenzi wake ambaye ni maarufu kwa jina la King bae 2 au Dark Stallion.

Mbali na kufuta picha hizo, pia Zari alishusha ujumbe mzito katika insta story yake ambao umeibua wasiwasi kwa wafuasi wake milioni 9.3 kuhusu mustakabali wa uhusuano wake ulianza kung’oa namba Februari mwaka huu.

Zari ambaye anaishi Afrika Kusini pamoja na watoto wawili wa Mondi, aliandika ujumbe huu kwenye insta story yake, “Nimemmisi lakini inanibidi nimuache aondoke. Kwa sababu kama hanijengi, hana faida kwangu siwezi kuendelea…,”

Kufuatia hali hiyo baadhi ya mashabiki wamedai kuwa hii inaweza kuwa muda muafaka kwa Mondi kurudisha majeshi kwa Zari baada ya Dark Stallion ambaye alikuwa raia wa Nigeria kutimuliwa.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments