.

8/09/2021

Ajinyonga Baada ya Kuachwa na Mkewe

Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Philemon Tandu (50) Mkazi wa Kijiji cha Ng’wandakw kata ya Haydom wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara amefariki dunia kwa kujinyonga baada ya kuachwa na mke wake akiwa na watoto watano.

 

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, kamishna msaidizi (ACP) Marrison Mwakyoma amesema tukio hilo limetokea juzi kwenye ambapo Philemon Tandu alijinyonga kwa kutumia kamba ya katani shingoni karibu na nyumba yake baada ya mkewe Christina Elia (45) kumuacha akiwa na watoto watano akisema hamtaki tena.

 

Kamanda Mwakyoma amesema chanzo cha kifo hicho ni matatizo ya familia kwani mara baada ya Tandu kuachwa na mkewe walijaribu kusuluhisha ugomvi wao ili wasiachane na walee watoto wao ila ikashindikana mwanamke huyo akaondoka.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger