.

8/17/2021

Aliyekuwa mkuu wa Mkoa Mbeya John Mwakipesile afariki duniaMbeya. Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwenye Serikali ya awamu ya nne, John Mwakipesile amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Agosti 17, 2021.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya Simu, Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Ismail Mlawa amesema wamepokea taarifa za msiba huo kwa masikitiko makubwa.

"Tumepata taarifa na sasa naelekea nyumbani kwa marehemu kujua taarifa zaidi na nitaweza kukuunganisha na familia ya marehemu kwani mimi sio mzungumzaji wa familia," amesema Mlawa.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jacob Mwakasole naye amethibitisha kupokea taarifa za msiba wa Mwakipesile na kwamba ni pigo kubwa kwao. Ameongeza kuwa hakuwa na taarifa za kuugua kwa Mwakipesile.


 
"Ni kweli nimepokea taarifa za msiba huo mkubwa wa baba yetu na kada wa chama. Chama tunataratibu zetu, tutashirikiana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo kumsitili marehemu Mwakipesile,” amesema mwenyekiti huyo.


Princes Mwaihojo, mdau wa maendeleo Mkoa wa Mbeya amesema watamkumbuka marehemu kwa namna alivyoupigania mkoa huo kuvutia na kupata wawekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger