Aly Ahly Wafungukia Usajili wa Luis

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



KOCHA Mkuu wa Al Ahly ya Misri raia wa Afrika Kusini, Pitso Mosimane, amemfungukia kwa mara ya kwanza aliyekuwa winga wa Simba, Luis Miquissone kuwa ni mchezaji hatari kutokea Afrika kwa
sasa na ndiyo maana amemsajili kwenye kikosi chake.


Luis aliyejiunga na Simba, Januari 2020, akitokea UD Songo ya kwao Msumbiji, mwishoni mwa msimu huu aliachana rasmi na timu hiyo kisha kujiunga na Al Ahly kwa mkataba wa miaka mitatu.

 

Taarifa kutoka nchini Misri, imeeleza kuwa, tangu Luis ajiunge na klabu hiyo amekuwa gumzo kubwa, jambo ambalo limewafanya waandishi wa nchini humo kumuuliza kocha Mosimane juu ya uwezo wake na kujikuta akimmwagia sifa lukuki.



“Miquissone ni mchezaji mzuri sana, ambaye nimemfahamu tangu akicheza kwao Msumbiji kisha kujiunga na Simba, hivyo hadi leo naamua kumsajili ni wazi nimejiridhisha ukubwa wa uwezo wake na kuona namna atakavyotusaidia.

 

“Niliwahi kumsajili huko nyuma lakini nikamtoa kwa mkopo, jambo mbalo baadaye baada ya kumuona Simba, alinishangaza sana kwa uwezo wake mkubwa, kwani alikuwa ni chachu ya ubora wa Simba na ndiyo maana sasa ameungana tena na sisi,” alisema Mosimane.

Stori: Musa Mateja,Dar es Salaam
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad