.

8/26/2021

Amos Makalla "Ilifanyika Busara Kummaliza na Risasi Japo Angekuwa Hai Angetusaidia Kujua Mambo Mengi"“Mkoa upo salama na shwari, tukio la jana kama lilivyotokea tulilidhibiti na pongezi kwa Jeshi la Polisi Tanzania, kama aliua Watu wanne na wengine ni Majeruhi kama tungesema tutumie busara ya kumuacha akiwa hai angeweza leta madhara zaidi'

“Ni kweli kama tungemdhibiti akiwa hai angetusaidia kujua mambo mengi lakini tayari alikua na silaha kubwa mbili, alikuwa mbioni kukimbia eneo la tukio, pangetokea madhara makubwa zaidi kama angeendelea kuachwa, hivyo ilitumika busara kufanya kile kilichotokea”

"Ni kweli tukio la jana lilizua taharuki, kama mlifuatilia nilitoa tamko la kusema tukio lile limeshadhibitiwa na Wananchi waendelee na shughuli zao kama kawaida hali ni salama na vyombo vya ulinzi na usalama wapo katika uchunguzi wa kina na taarifa itatolewa ya tukio"——— asema Mkuu ws Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla via Clouds360
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger