.

8/17/2021

Aunt Amchimba Mkwara Ruby

BADO habari nzito mjini ni patashika nguo kuchanika kati ya mwigizaji wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel na mwanamama anayekiwsha kunako Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’.


Wawili hao wanadaiwa kuingia kwenye vita kali baada ya kubadilishana wanaume waliozaa nao kwa maana ya Aunt kumchukua Kusah na Ruby kumbeba juujuu Moze Iyobo.

 

Hata hivyo, ukweli wa mambo ni kwamba, Aunt hajapendezwa hata kidogo na kitendo cha Ruby kumchukua Moze kwa sababu anaona kama anamchoresha hivyo amemchimba mkwara mzito.

Kupitia Insta Story zake, Aunt ameendelea kurusha vijembe na mikwara kama yote huku akimuomba Mungu kumzuia kwa sababu anaweza kujikuta akiozea jela.

 

“Nakwenda kumuacha Mungu arekebishe kila kitu kwa sababu nikirekebisha mwenyewe, basi jela itanihusu,” imesomeka moja na vijembe hivyo.Wengi wametafsiri ujumbe huo kuwa, uliwalenga Ruby na Moze Iyobo kwani ndiyo watu ambao ameendelea kujibizana nao kwa wiki ya pili sasa kwa madai kuwa wamekuwa wakimrusha roho na kumkosesha amani.Hata hivyo, ni kweli kwamba Ruby na Moze Iyobo wamekuwa wakioneshana mahaba ya hatari huku wakiambiana maneneno matamumatamu yanayodaiwa kumuumiza Aunt moyo wake.

 

Katika hali kama hiyo, vyanzo vya ndani ya familia ya Aunt vimeliambia Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuwa, pamoja na kwamba, mwanamama huyo yupo na Kusah, lakini bado roho yake ipo kwa Moze Iyobo ambaye amezaa naye mtoto wao wa kwanza aitwaye Cookie.

 

Kufuatia kuujua udhaifu huo wa Aunt, imedaiwa kwamba Ruby ameendelea kumpiga kwenye mshono kwa kuwa anajua hilo ndilo linalomuumiza hivyo anachokifanya ni kufanya sarakasi za mahaba na Moze Iyobo ili tu kumkomesha Aunt ambapo hali imeendelea kuwa mbaya juu ya maelewano kati ya familia hizo mbili.

 

Aunt alitua kwa Kusah na kuzaa naye mtoto mmoja wa kiume baada ya kutengana na Moze Iyobo ambaye naye alizaa naye mtoto mmoja wa kike.Kwa upande wake, Ruby anakiri kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi wa siri na Moze Iyobo kwa tariban miaka miwili sasa baada ya kutengana na Kusah ambaye alizaa naye mtoto mmoja wa kiume.

STORI; MWANDISHI WETU
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger