.

8/04/2021

Bastola ya DC Yakamatwa Ikitumika Kufanya Uhalifu Mbeya
JESHI la Polisi mkoani Mbeya linawashiklilia watu 5 kwa tuhuma za kukutwa na bastola moja na risasi 11, mali ya Mkuu wa wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, John Palingo ambayo wanadaiwa wamekuwa wakiitumia kufanya matukio ya uhalifu wa kuvunja nyumba na kuwapora mali za wananchi.

 

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei ameyasema hayo wakati akizungumza na wandishi wa habari katika kituo kikuu cha polisi jijini Mbeya.

 

Katika hatua nyingine kamanda Matei amesema jeshi la polisi limepata taarifa za kiintelijensia kuhusu watu wanaojipanga kufanya maandamo jijini Mbeya, na kutoa onyo kali kwa watu hao.

 

Kamanda Matei ametoa wito kwa wananchi mkoani Mbeya kutoa taarifa za uhalifu na walifu ili hatua ziweze kuchukuliwa na kuhakikisha watu wanaishi kwa amani na utulivu.

 
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger