.

8/18/2021

Binamu Bananga Awashukia Kina Gwajima "Wote Mna Makosa"Ujumbe unasomeka hivi 👉"MAGWAJIMA;

Wote mna makosa.

#Askofu;

Umepata kona ya kupaa kiumaarufu na umeitumia haswa, ila umewavunjia wakuu wako heshima. Kuonyesha kuna dalili za rushwa ktk mchakato wa kuleta chanjo UNAHITAJI MBAVU NENE KUJITOA KWENYE HILI. Kama huna ushahidi Baba Askofu umepishana na gari la mshahara.

Lakini liache kanisa lihubiri utukufu wa Mungu, kujisifu kuwa unawapiga bungeni kanisani sio sifa. Baki na hoja bungeni ambako pia una kinga lakini pia unaweza kushawishi chombo hicho cha kutunga sheria kikaelewa mtazamo wako na kukuunga mkono. Usiwavuruge waumini.

Ila imani yako ni imani ya serikali hii hii kipindi cha mwendazake walizizungumzia vibaya chanjo hizo hizo zinazoaminishwa sasa ni salama. Mkanganyiko uliletwa na wakuu. Hoja ni kukubaliana kutokukubaliana kistaarabu na ikibidi wakubwa wenye ushawishi kwenye jamii ya kitanzania wakutanishwe washawishiane KUKUBALIANA WOTE ama KUKATAA WOTE. Wakuu mnazidi kuwaumiza vichwa watanzania wengi wasio kuwa na ufahamu mpana.

#Waziri;
Kutumia makosa yaliyopita ya Askofu (uzinzi, uchadema, ufufuo) HUKO NI KUJISHUSHA KAMA DAKTARI. Kwamba unashindwa kuifundisha jamii uimara wa chanjo unatukumbusha mambo ya "mkono wa baunsa?" Kweli?

Sifa ya kiongozi ni kukabiliana na nyakati ngumu, na sasa shemeji yako kakuweka pagumu TUONYESHE UBORA WAKO. Vinginevyo wewe ni ktk waliofeli mapema. Jikumbuke wakati wa nyungu na michemsho ya ndimu na tangawizi ulivyoonyesha ubora kisha ujitafakari. KAMA ULIELEWESHWA UKAELEWA WAELEWESHE WENZIO SIO UBABE!

Inawezekana sijui itifaki lakini MAMLAKA YA KUYAAGIZA MAJESHI KUMSHUGHULIKIA SHEMEJI ni yako ama ulitakiwa kuomba hilo liagizwe na wenye mamlaka? Inawezekana kwa kuwa nchi hii wote ni kambale (wote wana sharubu baba, mama na watoto) mnadhani ni sawa tu kuvavanya.

MAGWAJIMA SAIDIENI JAMII
kama mna maugomvi yenu mengine msiutumie uwanja huu.

Mimi na familia yangu TUMECHANJA na TUNASHAWISHI WENGINE WACHANJE!
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

2 comments:

  1. huko kumuita hayati Magufuli mwendazake ndo kumekuondolea sifa ya kuwa msuluhishi mwema, unajua kutaja mabaya ya baba yetu, mbona husemi alituagiza tusali, nyungu, nk na hayo tulivuka ndo maana tupo?
    kwani Musa alifika Kanaani? mbona ndiye mwenye sifa ya kuwavusha wana wa israel?
    kuwa na moyo wa shukrani bwana!

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli umelezea vizuri Sana na Tena wafaa kuwa daraja Kati ya Hawa mashemeji,tatizo kwako Ni kumkejeli mpendwa wetu na kiongozi wetu wa awanu ya tano.Toa hoja zako vizuri utaeleweka tu 'mwenda zake ndio nn.

    ReplyDelete

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger