Breaking News "Messi Anaondoka Barcelona, Wenyewe Wathibitisha"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





TAARIFA zilizotolewa na Klabu ya Barcelona jioni hii zinaeleza kuwa, nyota wao Lionel Messi raia wa Argentina anaondoka klabuni hapo baada ya kushindikana kusaini mkataba mpya kutokana na sheria ya matumizi ya fedha ya La Liga.

Mtandao wa Barca umesema kuwa Klabu pamoja na Messi (34) mwenyewe wamefikia makubaliano hayo ya pamoja huku wakimshukuru kwa mchango wake mkubwa kwa klabu hiyo tangu ajiunge nayo akiwa mdogo na kumtakia maisha mema huko atakakokwenda ambapo PSG na Man City wanatajwa kuitaka huduma yake.

Messi ambaye anashikilia taji la Ballon d’Or mara sita, alikuwa amekubali kuongeza kandarasi ya miaka mitano Barca huku akikubali pia mshahara wake kupunguzwa kwa asilimia 50 baada ya mkataba wake wa awali kumalizika June 30, mwaka huu.

Messi ametumia asilimia kubwa ya maisha yake ya soka akiwa Barca kuanzia kwenye academy kabla ya kupandishwa timu ya wakubaa mwaka 2003, amecheza michezo 672 na kufunga mabao 778.

Barcelona wamwkuwa wakipitia maisha magumu ya kiuchumi kutokana na janga la corona hali inayowalazimu kwa sasa kupunguza bajeti yao ya msimu ujao kuendana na sheria ya LaLiga, pia wanapambana kuwapunguzia wachezaji wao mishahara ambao ni nahodhasaidizi Gerard Pique, Sergio Busquets na Sergi Roberto ambao wapo kwenyeazungumzo ya kupunguziwa asilimia 40 katika mikataba yao ijayo.

Pia wamejaribu kuwauza wachezaji wao kama Antoine Griezmann, Ousmane Dembele, Philippe Coutinho, Samuel Umtiti na Martin Braithwaite lakini hata wakifanya hivyo hali ni mbaya.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad