.

8/24/2021

Breaking News: Gwajima, Silaa Waondolewa Kamati Maadili
WABUNGE Josephat Gwajima (CCM, Kawe) na Jerry Silaa (CCM, Ukonga) ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Kinga na Mamlaka ya Bunge wameondolewa kwenye kamati hiyo hadi itakapoamuliwa vinginevyo.


Kamati ambayo wabunge hao wameondolewa, ndiyo inayowahoji kuhusu tuhuma mbalimbali zinazowakabili, ambapo jana Askofu Gwajima alifika mbele ya kamati hiyo na kuhojiwa na leo ni zamu ya Slaa ambaye naye anatarajiwa kufika na kuhojiwa.

Agosti 21, mwaka huu, Gwajima ambaye ni Mbunge wa Kawe (CCM) pamoja na Silaa, Mbunge wa Ukonga (CCM) waliitwa mbele ya Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger