.

8/17/2021

Breaking: Serikali Yaagiza Askofu Gwajima Akamatwe
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Doroth Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kumkamata na kumhoji Mbunge wa Kawe na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Mchungaji Josephat Gwajima ili athibitishe kauli  anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi  kuhusu chanjo   ya Covid-19.

 

Waziri Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne,  Agosti 17, 2021 akiwa katika kijiji cha Kyatunge Wilaya ya Butiama mkoani Mara na kueleza kuwa  Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za upotoshaji kwa makusudi kuhusu chanjo ya Corona jambo ambalo linaivuruga   wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo hatari duniani.

 

Maagizo hayo ya Waziri Gwajima yanakuja ikiwa nis aa chache tangu Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel kumtaka Askofu Gwajima kujitafakari juu ya madhara yatakayo wakuta wananchi kutokana na upotoshaji anaoendelea kuufanya na kuongeza kuwa hawezi kupingana na Serikali na hana uthibitisho wa kisayansi kuhusu chanjo ya corona.

 

“Gwajima amevuka mipaka, anapotosha Taifa, hawezi kupingana na serikali na hana uthibitisho wa kisayansi, anasema mtu akichanjwa kuna vitu vinaingizwa mwilini ili mtu afe baada ya miaka miwili ama kumi, tutamuita athibitishe hili, akishindwa tutamshughulikia.“Nimekuja kumuonya nikiwa kama mwana sayansi, ili ajue kwamba ametukanyaga sehemu, Gwajima anajua ukweli lakini ameamua kucheza ligi, tunamuonya tunataka awe na uthibitisho wa Kisayansi kwa kile anachosema kuhusu Chanjo ya Corona.


“Tumetumia nguvu nyingi sana kumuelimisha (Askofu Gwajima), tunataka tuthibitishiane kwamba sisi na yeye nani anataka kuiangamiza nchi, tujue nani anataka kuilinda nchi,” alisema Dk. Mollel.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

2 comments:

  1. Na serikali itoe udhibitisho kuwa chanjo ni salama

    ReplyDelete
  2. Na serikali idhibitishe chanjo ni salama na tukichanjwa hatutapatwa na maambukizi

    ReplyDelete

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger