BRELA Dar wajitokeza kupata chanjo ya UVICO -19

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



 
Pichani ni  baadhi ya Watumishi wa BRELA wakisubiri kupatiwa huduma ya chanjo ya UVICO-19 katika hospitali ya Jeshi la Magereza, Ukonga Jijini Dar es Salaam.
 

 


 Watumishi wa Wakala wa usajili wa biashara na Leseni (BRELA)  Agosti 13, 2021 wamejitokeza kwa wingi  kupata chanjo ya Uviko- 19  katika hospitali ya Jeshi ya Ukonga Jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo ni muendelezo wa kuitikia wito wa Serikali unaowataka wananchi   kujitokeza kwa hiari yao na kupata chanjo hiyo ya kujikinga na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Korona.

Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA  Bw. Godfrey Nyaisa akizungumzia zoezi hilo amesema ni muhimu kwa kila mtumishi kupata chanjo kuitikia maelekezo ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema pia kwakuwa gonjwa hilo linahatarisha usalama wa wasiochanja ikiwa ni pamoja na watumishi, familia  zao na jamii zinazowazunguka, siku zijazo kila mtumishi  wa BRELA atapaswa kuchanjwa.

Kwa upande wa watumishi waliopata chanjo wamemshukuru Afisa Mtendaji Mkuu Bw Godfrey  Nyaisa kwa   kutoa usafiri na  muda wa kazi kwa watumishi ili kwenda kupata chanjo hiyo.


Pichani ni baadhi ya Watumishi wa BRELA wakipatiwa huduma ya Chanjo ya UVICO -19 na Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Jeshi Ukonga, jijini Dar  es Salaam, Bibi Rachel Mulamula.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad